KISWAHILI F1 ANNUAL 2020
Ku-Download mtihani huu [ BOFYA HAPA ]
JAMHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA
OFISI YA RAIS
SERIKALI ZA MITAA NA
TAWALA ZA MIKOA
MTIHANI WA MUHULA WA
MWISHO
KIDATO CHA KWANZA
KISWAHILI
MUDA: Saa 2 ½
DEC, 2020.
Maelekezo:
-
Mtihani huu una sehemu A, B, C na D
-
Jibu maswali yote kwenye karatasi ya maswali
-
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
-
Dumisha usafi na uepuka kufutafuta ovyo ili
usipunguziwe alama utakazopata
SEHEMU A – UFAHAMU (alama 20)
1.
Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu maswali
yatakayofuata
Kwa hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza...............wengi
hawakuamini kuwa walichokisikia ndicho kilichokuwa kikitokea, hasa kwa wale
waliokosa fursa ya kuliona tukio hilo la kusikitisha kwa macho yao, hao ni wale
waliosikia sauti ya mirindimo iliyorindima mithili ya ngurumo za mvua.
Iliwawia vigumu pia kukubali kuwa sauti hizo zilizoshitua nyoyo na
kujenga taharuki miongoni mwa watu, ziliandamana na miale mekundu ya moto! Ndiyo maana watu hao waliendelea na shughuli
zao kama kawaida, punde matendo yao yalisimamishwa na mrindimo mkubwa uliozua
kishindo na kuthubutu kutingisha kuta, madirisha na hata kutiririsha mchanga na
vumbi jembamba kutoka kwenye mapaa ya nyumba zilizokuwa masafa fulani kutoka
kitongoji kilichokumbwa na mkasa huo.
Baada ya dakika chache walionekana raia wa vijiji vya jirani wakiwa kwenye hali ya mfadhaiko,
bila ya shaka walikuwa wakitafuta kimbilio la haraka ili kusalimisha maisha
yao. Ilikuwa kama mchezo wa
kuigiza.....................huyu anapenya hapa .............yule anatokomea
kule..............hawa wameshikana mikono, lakini wamepoteza matumaini...........ilimradi
mambo yalikuwa hayaelezeki kwa lugha ya kawaida.
Ingawa mtafaruku huo ulitawala kwenye nafsi ya kila aliyekuwa hapo,
lakini hali ya mandhari ya usiku huo ilikuwa na mvuto wa kupigiwa
mfano.....ukitupa macho mbinguni ulikuwa unatazamana na mawingu meupe
yaliyokuwa yakijikokota kwa mbwembwe
pembezoni, nyota nazo zilionesha ushirikiano
kwa kujimwaga moja moja na kumetameta
kwa zamu, mwezi nao haukuwa
nyuma kwani uliamua kufungulia nuru yake iliyokuwa ikiadhimisha maulidi
matakufu ya Mtume (rehema ziwe juu yake).
Hali hii ilikuwa ni faraja kwa wale waliotokomea vichakani au kwenye
viunga vya mji vilivyotelekezwa na mgao wa umeme ambao huzaa giza nene
lisilovumilika.
Kwa kuwa sakata hili
liliwakumbusha wananchi wengi kurejea kwa muumba wao angalau kwa saa chache,
kwa sala na maombi yaliyowasilishwa kwake kwa dhati na masikitiko ingawa
yalikuwa kwenye maneno yaliyosema kwa lugha tofauti tofauti za kikabila lakini
yalifika kwa maulana naye
akaridhia kwa kutoa majibu yaliyorudisha amani na utulivu iliyokuwa imepotea
kwa wastani wa saa tano hivi.
Kwa kila msamaria mwema hana budi kuwapa pole wakaazi wote wa Gongo la
Mboto na vitongoji vya jirani pamoja na kuwaunga mkono kwa hali na mali ili nao
waamini kuwa baada ya dhiki faraja, kutokana
na tukio la 05/08/2019
Maswali
i)
Pendekeza
kichwa cha habari kisichozidi maneno matano kisha ukiandike kwa herufi kubwa na
upigie mstari .......................................................................................................................................
ii)
Taja
methali iliyojitokeza kwenye aya ya mwisho ..............................................................................
iii) Taja maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika
kwenye kifungu
a)
Mbwembwe
..................................................................................................
b)
Kumetameta
.................................................................................................
c)
Sakata ...........................................................................................................
d)
Ngurumo
......................................................................................................
e)
Maulana .......................................................................................................
iv)
Tarehe 05/08/2019 kulitokea nini kwenye maeneo
yaliyotajwa katika habari uliyosoma?
......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
v)
Kihistoria tukio lililoelezwa kwenye kifungu
linakukumbusha kitu gani kilichowahi kutokea jijini Dar es Salaam
......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
vi)
Chagua jibu sahihi kati ya haya “watu waliodhurika
kutokana na tukio lililoelezwa kwenye kifungu wanaitwa”
a)
Wahanga
b)
Waathirika
c)
Watuhumiwa
d)
Wazembe
vii) Taja
madhara matano ambayo huwapata watu wanaofikwa na mkasa ulioelezwa kwenye
kifungu
a)
..................................................................................................................................................................................................................................................................................

SEHEMU B (alama 25)
UTUMISHI WA LUGHA NA USAHIHI WA WAANDISHI
2.
a) Sentensi
zifuatazo zimeandikwa kwa kukiuka kanuni za lugha. Ziandike upya ili kurekebisha makosa
i)
Mama inafanya kazi ofisini ....................................................................
ii)
Kasimu kazuri kamepotea
............................................................................................................
iii)
Mdada mmoja amepatwa na ajali ...............................................................................................
iv)
Juma haujambo? ..........................................................................................................................
v)
Jana tulicheza mpira kwa muda wa lisaa limoja.
.........................................................................
b) i) Lugha
ni ...................................................................................................................
....................................................................................................................................................................................................................................................................................................
ii) Kielezi huelezea kuhusu
a)
...........................................................................................................................

iii) Taja mambo mawili ambayo unaamini
yangetokea iwapo tusingekuwa na lugha kwenye jamii
a)
............................................................................................................................................................................................................................................................................

SEHEMU C (alama 25)
SARUFI
3.
a) Ainisha
maneno kwenye sentensi zifuatazo kwa kuweka alama ya neno husika chini yake
i)
Uzima wa mtu ni afya
.................................................................................................................
ii)
Penye mafanikio ndipo niendapo
..................................................................................................................
iii)
Watoto wangu hawa wawili warefu sana wamefaulu
................................................................................................................
iv)
Unanukia ingawa hauna ladha nzuri
..................................................................................................................
v)
Msaada wako umenifaa. Asante!
.................................................................................................................
b)
Sarufi ina dhima nyingi. Taja mbili kati ya hizo
a)
....................................................................................................................................................................................................................................................................................

c) Taja aina nne (4) za vielezi
i)
........................................................................................

SEHEMU D
FASIHI (alama 30)
- a) Tegua vitendawili vifuatazo
i)
Hausimiki
hausimami ........................................................................................................
ii)
Mzungu anamlamba Mwafrika
..........................................................................................
iii)
Pita huku nipite huku tukutane kwa mjomba
....................................................................
iv)
Wanangu wawili wanafukuzana lakini hawakutani ...........................................................
v)
Vibibi viwili viko mlimani
vyapeta.......................................................................................
b) Kauli zifuatazo zinamaana gani?
Mfano: Juma ameasi ukapera
Maana: Juma ameoa
i)
Chogo “ana mkono wa birika”
Maana:
.................................................................................................
ii)
Masanja “amefulia”
Maana:
.................................................................................................
iii)
Bwege hana “noma”
Maana:
.................................................................................................
iv)
Mshahara wenyewe “mkia wa mbuzi”
Maana:
.................................................................................................
v)
Huyu ndiye “mkali wao”
Maana:
.................................................................................................
c) Kamilisha
metheali zifuatazo
i)
Subira
............................................heri
ii)
Penye nia
.......................................................................................
iii)
.........................................pema
....................................panamwita
iv)
Chema ............................................kibaya
....................................
v)
Baniani ...........................
..........................chake ...........................